<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><title>Nilikupa Wewe Maisha Yangu TZR112</title>
<lyrics>[V1]
 Nilikupa wewe
 Damu ya moyoni,
 Ili wokolewe,
 Winuke ufuni:
 Nimekunyimani?
 Umenipa nini?

[V2]
 Nilikupa miaka
 Yangu duniani
 Upate inuka,
 Kuishi Mbinguni:
 Nimekunyimani?
 Umenipa nini:

[V3]
 Niliacha nuru
 Za Baba, Mbinguni,
 Kwingia taabu
 Za ulimwenguni:
 Nimekunyimani?
 Umenipa nini?

[V4]
 Niliteswa sana,
 Mateso kifoni,
 Usije yaona
 Hayo ya motoni:
 Nimekunyimani?
 Umenipa nini?

[V5]
 Nimekuletea
 Huku duniani
 Upendo na afya
 Zatoka Mbinguni:
 Nimekunyimani?
 Umenipa nini?

[V6]
 Nipe siku zako,
 Udumu mwangani;
 Na taabu yako,
 Wingie rahani
 Nafsi, pendo, mali,
 Twae Imanweli.</lyrics>
<hymn_number>112</hymn_number>
</song>